Sports/Michezo

Thomas Tuchel: Kocha wa Chelsea Ataja Sababu Zilizochangia Kufungwa na Leeds

sababu zilizochangia chelsea kufungwa na leeds
Written by admin

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel ametaja baadhi ya changamoto zilizokumba kikosi chake na kuchangia ushindi wa 3-0 kwa Leeds siku ya Jumapili, Agosti 21.

Itakumbukwa kuwa Blues ndiyo waligharamika zaidi wakati wa dirisha la uhamisho wakichomoa kima cha pauni 170 milioni.

Mahesabu ya mlinda lango Edouard Mendy yalishindwa kupangua hatari ya Brenden Aaronson na kumpa nafasi ya wazi kutinga bao la kwanza kabla ya Rodrigo kumuadhibu Raheem Sterling kutokana na masihara yake baada ya Muingereza huyo kupeana mpira wa bwerere.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, kocha wa Chelsea Thomas Tuchel wanahabari kwamba kitu kilichosababisha kilianza siku iliyotangulia kwani Hawakuwa na ndege ya kufika hivyo walitumia basi kwa usafiri na hivyo uchovu wa wachezaji ulichangia.

Katika taarifa tofauti, winga wa Chelsea, Christian Pulisic anaripotiwa kuwa kwenye mpango wa kuhamia klabu ya Manchester United msimu huu wa joto. Pulisic amekuwa akikumbana na wakati mgumu kuingia kwenye timu ya kwanza ya Blues chini ya ukufunzi wa Thomas Tuchel, na hivyo kumwacha bila budi ila kufanya uamuzi wa kuondoka.

Mzawa huyo wa Marekani amekuwa akitafuta nafasi ya kufanya mazungumzo na Tuchel kumueleza wazi iwapo anahitaji huduma zake.

Inaaminika kuwa kuwasili kwa Raheem Sterling kumeathiri sana nafasi yake kwenye klabu ya Chelsea na hivyo ikihofiwa kwamba huenda atakosa kuchezeshwa na kutupwa mkekani.

About the author

admin

Leave a Comment