News/Habari Uncategorized

Mbunge amkashifu Rais Kenyatta

Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri
Written by admin

Mbunge wa Bahati kimani Ngunjiri amemtaka Raisi Uhuru Kenyatta kuweka wazi kwa wakenya  kuhusiana na hatua anazonuia kufanya kuhusiana na swala nzima la kupanda kwa gharama ya maisha nchini.

Akiongea mjini Nakuru Ngunjiri amesema
kuwa  mwananchi wa kawaida ndiye anayeumia zaidi kutokana na hali
hii  akisema wengi wa wananchi  wanahudumu chini ya mapato ya
shilingi mia kwa sasa.

Aidha amesema kuwa  uwepo wa madeni makubwa ya nchi za kigeni ni miongoni mwa  baadhi ya hali hii akitaja mfano wa deni la nchini uchina anayosema  inakandamaiza  uchumi wa taifa

“Watu watakula reli kweli ?Rais anafaa kuelewa kwamaba yeye
ndiye aliyechaguliwa na wananchi “Ngunjiri alisema.

Na Sarah Nyangeri

About the author

admin

Leave a Comment