Katibu katika wizara ya elimu Belio Kipsang amekana madai kuwa kuna baadhi ya watahiniwa ambao wameathirika na kemikali aina ya Xylene ambayo inadaiwa kutumika wiki jana katika mtihani wa kitaifa somo la kemia.
Kipsang amesema kufikia sasa hamna kesi iliyoripotiwa na kutaka usaidizi ama idara ya elimu kushirikishwa nchini.
Wakati uohuo amesema kuwa maafisa wanaosimamia mitihani hiyo wako macho katika kuhakikisha hamna kesi za wizi wa aina yoyote ambao unashuhudiwa.
Kipsang alisema hayo wakati wa ziara yake ya kuangazia shughli nzima za mtihani wa kemia katika shule ya wavulana ya Nakuru, kaunti ya Nakuru.
Leave a Comment