Mratibu wa maswala ya watu wanaoishi na ulemavu katika kaunti ya Baringo Paul Chepkeitany anataka wazazi kuhakikisha kwamba watoto wote walio na ulemavu wanasajiliwa kikamilifu,ili waweze kupokea haki zao za kimsingi kama vile masomo.
Akihutubia hafla moja ya hadhara mjini Marigat siku ya jumatatu,Chepkeitany alisema watu walio na ulemavu wana mchango mkubwa katika ustawi wa jamii.
Mratibu huyo anasema watoto wengi walio na ulemavu bado wanafichwa manyumbani,ili hali afisi zinazopigania haki za walemavu zipo ange na tayari kutetea haki zao.
Leave a Comment