Watoto takribani 7,000 wanaugua ugonjwa usiojulikana nchini DRC, ugonjwa unaokuja na dalili za homa kali na kuharisha.
Mlipuko huo ulianza Agosti mwaka huu huku sampuli zikipelekwa katika Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Biolojia, mjini Kinshasa ili kubaini chanzo cha ugonjwa huo tarehe 7 mwezi huu.
Mgomo wa wafanyakazi wa matibabu katika Mkoa wa Kwilu ulichelewesha tahadhari ya mapema.
Watoto 286 walio chini ya miaka mitano walifariki katika kipindi cha miezi mitatu kutokana na ugonjwa ambao haukujulikana asili yake.
Mkuu wa kitengo cha afya cha jimbo la Kwilu Jean Pierre Baseke alithibitisha haya kwenye redio ya umoja wa mataifa katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo maarufu radio Okapi.
Alibainisha kuwa tangu mwishoni mwa Agosti ugonjwa huo ulipotokea, kumekuwa na zaidi ya maambukizi 7,000 sasa ikiwa ni pamoja na vifo 286. Dalili ni pamoja na homa na maumivu ya tumbo, kutapika na upungufu wa damu.
Leave a Comment