Mwanamuziki mashuhuri Esther Akoth almaarufu Akothee amefichua kuwa alitoroka nyumbani kwao na kuenda kuolewa akiwa na umri mdogo wa miaka 14 tu.
Mama huyo wa watoto watano amekiri kwamba hatua hiyo kwa kweli ilivunja moyo wa mzazi mke kwani alikuwa na matumaini makubwa naye.
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 42 alisema kuwa mapenzi yake kwa muziki na dansi yalipiku mengine yote lakini mamake alitia juhudi kumchunga na kumlea kulingana na maadili ya Kikristo.
Alifichua kuwa mzazi wake ambaye kitaaluma ni mwalimu hata alichukua hatua ya kumpeleka katika vituo kadhaa vya polisi baada ya kukatisha masomo yake ili aolewe akiwa na umri mdogo sana.
Akothee alifichua zaidi kuwa mamake hakupenda familia ambayo alitoroka kwenda kuolewa, ndiposa alimshinikiza sana arudi shuleni.
Hadi kufikia sasa msanii huyo bado anaogopa kuwatambulisha wapenzi wake wapya kwa mamake kutokana na ukali wake
Amesema mzazi wake anamtambua tu aliyekuwa mumewe wa kwanza na ambaye ni baba ya mabinti wake watatu, Jared Okello .
Leave a Comment