“Ninaanza kwa kukusanya kila kitu nilichonunua,” mcheshi na mtangazaji wa redio Oga Obinna amesema.
Haya yanajiri siku chache baada ya baby mamake kudai kumtendea vibaya na kufanya iwe vigumu kwao kulea binti zao kwa amani.
“Watu wabaki vile walipatwa. Una marupurupu ambayo ‘unayatumia vibaya. Mwache mwanamume wa sasa achukue usukani. Kitu pekee ambacho nitatoa ni chochote ambacho kinaathiri watoto wangu moja kwa moja,” aliongeza.
obinna alisema “Natukanwa hadharani, nachafuliwa hadharani, nachafuliwa hadharani na mnataka kuniunga mkono au kunitetea faragha. Kweli?? Sihitaji. Kama huwezi kusema ukweli wazi acha kunipigia simu,”.
Leave a Comment