Katika eneo la Molo ni visa vitatu ambavyo vimeripotiwa vya dalili za Covid-19 lakini vyote zimedhibitishwa kuwa nje ya hatari ya virusi hivyo.
Naibu Kamishina wa kaunti ndogo ya Molo David Wanyonyi amesema idara ya usalama pamoja na ile ya afya zinafanya kazi bega kwa bega ili kuhakikisha eneo hilo liko salama
Akiongea katika kikao na wanahabari Wanyonyi amesema serikali inaendelea kuratibu mipango ya kukabiliana na virusi vya covid-19
Huku hayo yakijiri…
Makao ya wazee mjini Nakuru yamechukua tahadhari mapema ya kuwakinga wazee dhidi ya homa hatari ya corona..Sarah Nyangeri ameongea na meneja msimamizi katika makao hayo na kuandaa ripoti ifuatayo
Usimamizi wa makao ya wazee mjini Nakuru umepiga marufuku wageni kwenye makao ya wakongwe hao sawa na kuzuia wazee hao kuondoka makaoni wakisema ni kwenye juhudi za kuzuia maambukizi ya homa ya corona.
Monica wanjiku ni Meneja msimamizi wa makao hayo viungani mwa mji wa Nakuru na amesema kuwa hatua hiyoni bora kuwazuia wazee hao dhidi ya homa hiyo angamizi ya corona.
Aidha, amesema kuwa wazee hao hawaruhusiwi kutoka kwenye makao hayo kutafuta huduma za afya akidokeza kuwa mikakati imewekwa ya kuwahudumia kikamilifu.
Kwa upande wa Wazee hao hofu yao kuu ikiwa maambukizi ya homa hiyo wakizingatia umri wao wa miaka sitini na kwenda juu na ambao umetajwa kuwa hatari kwa janga hilo la covid 19.
Sarah Nyangeri
Leave a Comment