Mwanamke mwenye umri wa makamu mama wa watoto watatu anatarajiwa kufunguliwa mashtaka baada ya kupatikana akimdhulumu mjakazi wake mwenye umri wa miaka 16 katika eneo la Muguga Pipeline viungani mwa mji wa Nakuru.
Hellena Kabukuru OCPD wa Nakuru Mashariki amethibitisha hili na kusema kuwa alipokea ripoti kutoka kwa wasamaria wema na majirani ambao walishuhudia mjakazi huyo akiwa amevunjika mkono mbali na kuwa na kidonda kwenye uso wake majeraha yanayoaminika kutokana na kichapo alipopokea kutoka kwa mwajiri wake wa mwaka mmoja Susan Wangeci..
Kabukuru anasema Mwajiri huyo atafunguliwa mashtaka pale uchunguzi utakamilishwa huku msichana huyo kwa sasa akipelekwa katika hospitali kuu ya jimbo kwa matibabu.
Kwa mujibu wa OCPD Wangeci atafunguliwa mashtaka ya dhulma sawa na kuajiri mtoto mwenye umri mdogo na hivyo kumnyima haki zake za kuwa shuleni.
Juhudi za kuifikia familia yake hazijafua dafu.
Sarah Nyangeri
Leave a Comment