Serikali za kaunti pamoja na ile ya kitaifa zimetakiwa kutenga raslimali zitakazotumikia kukuza talanta za watu wanaoishi na ulemavu nchini.
Wito huo ulitolewa na wasanii wasio na uwezo wa kuona kutoka Wanyororo Bahati, wakisema talanta nyingi zimekuwa zikipotelea mashinani bila ya yeyote kuzitambua.
Wakiongozwa na Lucy Gitama, wasanii hao walisema kuwa serikali ina uwezo wa kukuza talanta hizo na kuwawezesha watu wanaoishi na changamoto za maumbile kujiinua kimaisha.
Leave a Comment