Mbunge mwaakilishi wa akina mama kaunti ya Baringo Gladwel Cheruiyot ametoa wito kwa wananchi kupuuza uvumi ambao unaenezwa kuhusu chanjo dhidi ya Covid 19, kuwa ina athari kwa afya ya uzazi na maisha ya baadaye.
Akihutubu katika hafla moja ya hadhara katika eneo la Mogotio,Gladwel anadai kwamba wakongwe katika maeneo ya Baringo wanazidi kufariki kwa kukosa kupokea chanjo hiyo,kwani idadi kubwa ya wananchi hawajakumbatia chanjo hiyo.
Mwanasiasa huyo anasema wananchi wanafaa kuiga mfano wa Rais Uhuru Kenyatta ambaye tayari amepokea chanjo hiyo.
Leave a Comment