Wanabodaboda mjini Nakuru, wameitaka serikali ya kaunti hiyo kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wahudumu wenzao ambao hawajajisajili na wamekuwa wakiwabeba wateja na kuwaibia.
Wakizungumza na kituo hiki,wahudumu hao walisema pikipiki hizo hazina nambari za usajili na zimekuwa zikitumika na wezi kuendeleza uhalifu katikati mwa mji wa Nakuru.
Wameongeza kuwa,wamekuwa wakikamatwa wakihusishwa na wizi,huku kwa sasa wakisema serikali ya kaunti ya Nakuru imesalia kimya kuhusiana na swala hilo, licha ya malalamishi kutolewa.
Leave a Comment