Aliyekuwa Gavana wa kaunti ya Baringo Benjamin Cheboi anataka bunge la kaunti hiyo kubuni sheria kuhusu afya kwa wakongwe kwenye jamii, ili kuondoa mzigo wa kuchanga pesa za kugharamia matibabu yao.
Akiongea kule Koibatek Cheboi alisema matibabu kwa wakongwe yanafaa kutolewa bila malipo, na kuhimiza bunge la kaunti hiyo kuhakikisha kwamba sheria kuhusu bima ya afya kwa wakongwe inabuniwa.
Aidha wanasiasa wengi katika maeneo ya Baringo wanazidi kuwa tegemeo na kimbilio kwa watu wanaotafuta matibabu na pia shughuli za mazishi.
Leave a Comment