Chama cha muungano wa wafanyakazi (COTU), Leo Alhamisi Septemba 16 2021, kimepinga ongezeko la bei ya mafuta kikiishauri serikali kutafuta mbinu za kibunifu za kutanua wigo wa mapato.
Katika taarifa yao chama hicho kupitia katibu wake mkuu, Francis Atwoli, kinamtaka rais Kenyatta kujitokeza na kutoa maelezo sababu za mamlaka ya udhibiti wa kawi na petroli kuongezea bei ya mafuta kwa kiasi kikubwa.
Atwoli alisema ongezeko hilo limekuja wakati wafanyakazi wengi wanatetereka kutokana na utozwaji mkubwa wa kodi pamoja na kupunguziwa mishahara kisa janga la korona.
Mamlaka hiyo iliongeza bei ya petroli kwa sh. 7.58, mafuta ya dizeli na yale ya taa kwa sh. 7.94 na sh. 12.97 mtawalia. Ongezeko ambalo Atwoli anataja kuwa lisilo zingativu na kusema litaathiri pakubwa bidhaa za mahitaji ya msingi.
Leave a Comment