Idara ya magereza katika eneo la Eldama Ravine kaunti ya Baringo itazidi kutoa ushauri kwa maafisa wa kitengo hicho ,ili kuzuia visa vya maafisa wa idara hiyo kujitoa uhai.
Akizungumza na wanahabari baada ya afisa mmoja wa gereza la Eldama Ravine kujitoa uhai, Afisa mkuu wa gereza la Eldama Ravine Francis Kimani anasema idara hiyo imebuni mikakati za kusuluhisha matatizo ya maafisa wake,kwani baadhi yao wanapitia tatizo la uhaba wa pesa,baada ya mishahara yao kukatwa ili kugharamia mikopo wanazodaiwa na benki.
Leave a Comment