Gavana wa Elgeyo Marakwet, Alex Tolgos amehojiwa kwa zaidi ya saa mbili na maafisa wa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC .
Akizungumza na wanahabari baada ya kuhojiwa na makachero wa EACC, Tolgos amesema amehojiwa kuhusu matumizi ya shilingi takribani elfu mia saba na elfu arubaini za ununuzi wa mafuta yaliyotumika kwenye magari ya hospitali zikiwamo ambulensi, kuanzia mwaka wa 2013 hadi mwaka wa 2016 katika kaunti hiyo.
Wakati uo huo, Tolgos amepuuza taarifa za awali kwamba anachunguzwa kuhusu utoaji tenda wa kununua mafuta ya shilingi milioni mia mbili kutoka kwa kituo cha mafuta kinachodaiwa kuwa chake.
Amesema hana lolote la kuogopa kwani uchunguzi unaondelea ni miongoni mwa majukumu yaliyotwikwa ofisi ya gavana kufafanua kuhusu matumizi ya fedha katika kaunti.
Leave a Comment