Wapelelezi na wataalamu wa moto wametumwa katika soko la Gikomba kuchunguza kisa kingine cha moto uliotokea usiku wa kuamkia leo.
Moto huo uliteketeza mali ya mamilioni ya pesa katika soko hilo kubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashiriki.
Polisi walisema vibanda na nguo zilizokuwa kwenye ardhi ya ukubwa wa ekari tatu ziliteketezwa na moto huo uliozuka mwendo wa saa sita usiku.
Wafanyibiashara wachache tu ndio waliweza kuokoa mali yao kwani moto ule ulienea kwa kasi mno ukiteketeza kila kitu kilichokuwa katika eneo lililoathirika.
Chanzo cha moto huo bado hakijatambulika.
Haya yanajiri saa machache tu baada ya mahakama kuruhusu huduma ya jiji la Nairobi (NMS) kufurusha baadhi ya wauzaji wa Mitumba katika soko hilo ili kupatia nafasi upanuzi wa zahanati ya Pumwani Majengo.
Moto huo umekuja wakati ambapo serikali iliahidi kuweka kamera za CCTV ili kushughulikia matukio hayo ya mara kwa mara. Tukio kama hilo lilitokea mahali hapo mwezi uliopita.
Leave a Comment