Inspekta generali wa polisi Hillary Mutyambai amewaonya wananchi dhidi ya kuandamana wakati huu wa janga la korona.
Kulingana na Mutyambai suala la maandamano linakwenda kinyume na mikakati ya kuzuia maambukizi zaidi ya korona kama inavyosahuri na wizara ya afya.
Haya yanakuja baada ya wananchi kwenye mtandao wa Twita kutaka majibu kuhusiana na kukamatwa kwa wanaharakati wanao andamana kulalamikia kufujwa kwa pesa za kukabiliana na janga la korona nchini.
Haya yanakuja wakati ambapo wanaharakati nchini wakizuiliwa kwenye kaunti ya Nakuru na Nairobi kwa madai ya kuandama kushinikiza serikali ya kitaifa na wizara ya afya kuelezea zilikokwenda pesa zilizotolewa na wafadhili kukabiliana na janga la korona.
Leave a Comment