Huduma katika hospitali kuu ya kaunti ndogo ya Naivasha zimeendelea kufifia baada ya ongezeko la miili ambayo haijachukuliwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo.
Kwa sasa kuna miili ishirini ambayo haijachukuliwa huku Mochari hiyo ikiwa na uwezo wa kuhifadhi miili kumi na miwili pekee kwa wakati mmoja.
Kulingana na wasimamizi kutoka idara ya afya na usafi wa umma, walikuwa wakifanya mipango ili kuweza kuizika miili hiyo katika kaburi la pamoja huko Longonot.
Hatua hiyo imejiri miezi mitatu baada ya shughuli ya kuizika miili kumi na sita katika kaburi hilo kufanyika baada ya miili hiyo kuhifadhiwa kwa zaidi ya muda unaokubaliwa kisheria.
NA SILAS MWITI
Leave a Comment