Mwanafunzi wa darasa la sita anazuiliwa na maafisa wa polisi kwa kumuua mwenzake kutokana na mzozo wa Ugali na Kunde, na kisha kuutupa mwili wake katika mto wa Simakina, Navakholo kaunti ya Kakamega.
OCPD wa Navakholo Richard Omanga alidhibitisha hayo akisema mtoto aliyeuwawa alikuwa na umri wa miaka kumi, na alivaamiwa na mwenzake wakati akichunga mifugo ya wazazi wake.
Omanga aliongeza kwamba, mzozo uliibuka wakati mshukiwa alitoka shuleni jana na kufahamishwa kwamba chakula alichokuwa amehifadhiwa, kilikuwa kimeliwa na mwenzake huyo ambaye ni jirani yao.
Mwanafunzi huyo alimsaka mwenzake na kumgonga kwa kifaa butu kichani kisha kuutupa mwili wake mtoni, kabla ya kwenda shuleni asubuhi ya leo na kujiripoti kwa waalimu.
Baadaye aliwapeleka katika eneo la tukio ambapo waliupata mwili wa mwanafunzi huyo, OCPD Omanga akisema mwili huo ambao kwa sasa upo kwenye makafani ya hospitali ya rufaa ya Kakamega ulikuwa na majeraha mabaya kichwani.
Leave a Comment