Kampuni zinazotoa mikopo kwa njia ya mitandao na simu zitalazimika kutii sheria zinazolinda data ya wakenya lau sivyo zinahatarisha kunyaganywa leseni, ikiwa marekebisho ya mswaada wa benki kuu ya Kenya (Central Bank (Amendment) Bill 2021) yatapitishwa bungeni.
Mwishoni mwa wiki jana kamati ya bunge kuhusu fedha na mipango ya kitaifa, iliitaka benki kuu ya Kenya CBK kushirikiana na mamlaka ya mawasiliano nchini CA na ofisi ya kamishna wa ulinzi wa data, katika kukagua kampuni hizo za utoaji mikopo ili kuhakikisha zinatimiza sheria ya usiri wa data.
Mwelekeo huo huenda ukapunguza malalamishi ya wakenya ambao data kuhusu mikopo wanayochukua imekuwa ikianikwa wazi kwa marafiki, familia na waajiri wao na kampuni zinazotoa mikopo hiyo.
Leave a Comment