Mlinzi wa hospitali ya Njoro, kaunti ya Nakuru, aliyekuwa kwenye zamu usiku wa jana wakati afisa wa Polisi Bernard Sivo alimvaamia mpenziwe na kumuua kwa kumpiga risasi, alijitokeza kuzungumzia yaliyojiri wakati wa kisa hicho.
Mlinzi huyo kwa jina Vincent Lematoo alisema afisa huyo wa polisi hakuwa na haja ya kuangamiza au kudhuru mtu mwingine yeyote, ila alilenga mhasiriwa Mary Nyambura aliyekuwa amelazwa baada ya kuvunjwa mguu na afisa huyo hapo awali mwendo wa saa tatu.
Hayo yalidhibitishwa mapema leo na OCPD katika eneo la Njoro Jonathan Kisaka akisema baada ya afisa huyo kumuua mpenziwe alielekea hadi kwenye kituo cha polisi na kukiteka nyara kwa mda kabla ya kujiua.
Leave a Comment