ODM imetimiza ahadi yake na kutoa shilingi milioni 117.2 kwa washirika wake wa zamani katika uliokuwa muungano wa NASA. Fedha hizo zimetolewa kwa vyama vya WIPER na ANC.
ODM hata hivyo, imezuilia Shilingi milioni 36 za Ford Kenya ambayo inakabiliwa na malumbano ya uongozi.
Fedha hizo zilikuwa sehemu ya mgao wa vyama vya siasa ambao chama hicho kilikubaliana mwezi uliopita kugawanya na washirika wake wa zamani.
Afisa mmoja wa cheo cha juu katika ODM amethibitisha kwamba walihamisha pesa hizo kwa akaunti za Wiper na ANC wiki iliyopita.
Leave a Comment