Serikali kuu itaanza kuwapa msaada wa chakula na maji wanaoathiriwa na njaa ili kuokoa maisha yao.
Haya yanajiri baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutaja baa la njaa kuwa janga la taifa kwa mujibu wa naibu Waziri wa Ugatuzi na Maeneo Kame Gideon Mung’aro.
Mung’aro pia alidokeza kuwa mawaziri Eugene Wamalwa, na maafisa wengine serikalini wataanza kuzunguka sehemu mbali mbali nchini kuhakikisha Wakenya wanapewa vyakula na maji ili wasife kwa njaa.
Hata hivyo, kiongozi huyo amewataka viongozi wa pwani kuweka mikakati ya kuhakikisha uwepo wa chakula kukabiliana na swala la ukame.
Aidha, wakazi wa maeneo kame wameendelea kulalama kuhusiana na kuchelewa kwa zoezi la kutoa chakula.
Leave a Comment