Jambazi
mmoja aliyekuwa amejihami kwa kisu kufanya uhalifu katika eneo la Muguga,
kaunti ya Kiambu alipoteza maisha yake baada ya kuwezwa nguvu na mhasiriwa wake
mmoja ambaye alimpokonya kisu chake na kukitumia kumuua.
Evans
Atuya (35) alikuwa ameandama na majambazi wenzake wawili kushambulia nyumba ya
Godwin Wanyama mida ya saa nane usiku wa kuamkia Jumapili bila kufahamu kuwa
siku yake ya arubaini ilikuwa imewadia.
Kulingana
na DCI, watatu hao walitumia jiwe kubwa kuvunja mlango wa nyumba ya Wanyama ili
wapate kuingia ndani kuiba ila mwenye nyumba akaamshwa na kelele zile na hapo
kizaazaa kikaanza.
Wanyama ambaye alikuwa amejitolea mhanga kulinda mali yake alikimbilia mkono wa Atuya kwa busara na kumpokonya kisu kisha bila kupoteza mda akamdunga nacho shingoni. Anytime online slots, play online slots, treasure island resort and casino map online casinos, mobile casinos, mobile slot games, and Mobile gambling.
Wenzake kuona kilichokuwa kimemtendekea mwenzao wakatimua mbio na kutoweka . Atuya alijaribu kuwafuata wenzake huku damu ikiwa inamtoka shingoni ila akaanguka na kufariki papo hapo baada ya kupiga hatua chache tu.
Majirani ambao walikuwa wamemshwa na kelele ghasia ambazo zilikuwa zimetokea walijumuika kumsaidia Wanyama ila wakapata alikuwa ashadhibiti tukio hilo.
Polisi kutoka kituo cha Muguga walifika katika eneo la tukio na kufanya uchunguzi ili kuthibitisha yaliyokuwa yametokea.
Mwili
wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya
Gachie huku msako dhidi ya majambazi ambao waliweza kutoroka ukianzishwa.
Leave a Comment