Wanafunzi wachanga wapatao 36, 000 wanatarajiwa kunufaika na mpango wa lishe shuleni uliozinduliwa na serikali ya kaunti ya Kiambu, katika juhudi za kukabiliana na utapiamlo na pia kuwapa motisha wanafunzi.
Mpango huo utakaogharimu shilingi milioni 52, uliozinduliwa na Gavana wa Kaunti hiyo James Nyoro, utatekelezwa katika vituo vyote 528 vya elimu ya chekechea katika kaunti hiyo.
Wanafunzi hao watapewa uji ulio na virutubishi kuanzia siku ya Jumatatu hadi Ijumaa, kupitia mpango huo endelevu ambao Nyoro alisema umefadhiliwa vilivyo kupitia washirika.
Washirika katika mpango huo ni pamoja na chuo kikuu cha JKUAT, wanaohakikisha Unga huo wa uji una virutubishi vya ubora wa hali ya juu ili wanafunzi wawe na afya bora.
Wazazi walipongeza mradi huo, wakisema utasababisha watoto wengi kwenda shuleni.
Leave a Comment