Mtoto msichana mwenye umri wa miaka 8 kule majengo, Kilgoris ameaga dunia baada ya kugongwa kimakosa na babake wakati wazazi wake wakigombana nyumbani kwao.
Mwanamume huyo anayejulikana kama Amos Maenga (30) alikuwa analenga kumgonga mkewe Esther Kaiseyi (21) kwa kifaa butu, ila akakosea na badala yake kumgonga kichwani mwanawe na kumjeruhi vibaya.
Wawili hao walimkimbiza mtoto wao katika hospitali ya kaunti ndogo ya Kilgoris ambapo alifariki akipokea matibabu kulingana na taarifa ya DCI.
Wazazi hao wanazuiliwa kwenye kituo cha polisi cha Kilgoris huku uchunguzi ukiendelea.
Leave a Comment