Gavana wa Kilifi Amason Kingi amekaribisha uamuzi wa chama cha ODM kumtengua katika nafasi ya mwenyekiti wa kaunti ya kilifi. Nafasi yake ikichukuliwa na mbunge wa Ganze Teddy Mwambire.
Katika taarifa aliyotoa kwa vyombo vya habari Kingi alimshukuru kinara wa ODM Raila Odinga kwa kumpa nafasi kuwa mwenyekiti wa chama hicho kaunti ya Kilifi kwa muda wa miaka tisa.
Kingi alisema chini ya uongozi wake kama mwenyekiti wa ODM chama hicho kilitoa ushindani mkali kwa vyama vingine haswa kwenye uchaguzi mkuu uliopita
Gavana huyo alishtumiwa kwa kutotii chama na kujihusisha na chama kipya.
Amekuwa akilaumiwa kwa kuongoza juhudi za kuundwa kwa chama cha wapwani kwa jina Jumuia, ili kuwa na msukumo mmoja kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Leave a Comment