Wakulima wa ngano hapa nchini, Kenya, watanufaika endapo sera mpya inayolenga kuinua bei ya zao hilo itapitishwa.
Kulingana na halmashauri ya kilimo na chakula nchini AFA, sheria hiyo inayodhibiti bei za uuzaji wa zao hilo itashuhudia wakulima wakiuza ngano gunia moja ya kilo tisini kwa shilingi 3,700 badala ya bei ya sasa ya shilingi 1,800. Enter in a search query https://nikel.co.id/21383-casino-ridge-rd-yorba-linda-ca/ into MP3-Wolf and start the program, and if you lose.
Akihutubia wakulima wa ngano mjini Narok Mkurugenzi mkuu wa AFA Kello
Harsama, amesema bei hiyo ya shilingi 3,700 kwa mfuko wa kilo 90 wa ngano,
iliafikiwa kati ya wasagaji ngano na wakulima katika juhudi za kuwapa motisha
wakulima kuongeza ukuzaji wa zao hilo huku kaunti hiyo ikizalisha asilimia kumi
tu ya ngano inayotumiwa hapa nchini.
Kaunti ya Narok hadi kufikia sasa imevuna magunia 300,000 ya ngano mwaka huu
na inatarajia kuvuna magunia mengine 250,000 zaidi.
Leave a Comment