Mwanamme mwenye umri wa miaka 23 amejitoa uhai kule Mwingi baada ya kushikwa na msongo wa mawazo uliochangiwa na kuibiwa kwa pikipiki yake ya boda boda.
Nicholas Nzau ambaye alikuwa mchuuzi alijitoa uhai jioni ya jana kwenye nyumba aliyokodi kulingana na mkewe Ruth Mwikali.
Mwikali alisema alikuwa amemwacha mume wake na mtoto wao wa miezi minne na kwenda kazini na aliporudi akapata mlango umefungwa na simu yake haikuwa inajibiwa.
Alipomtafuta kwa marafiki na kumkosa ndipo akaamua kuvunja mlango na kukutana na mwili wa mume wake, huku mtoto wao wa kiume akiwa kitandani akilia.
Mwikali alisema mume wake alinunua pikipiki hiyo kwa shilingi 140,000 ili kumsaidia katika kazi zake za uchuuzi wa bidhaa.
Leave a Comment