Aliyekuwa waziri wa kilimo ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Service Party-TSP Mwangi Kiunjuri, ametoa wito wa kurejeshwa kwa polisi wa akiba katika eneo la Laikipia kufuatia msururu wa mashambulizi ya majambazi.
Kiunjuri amesema hayo saa chache tu baada ya serikali kutangaza kafyu ya saa kumi na mbili jioni hadi saa kumi na mbili alfajiri kwenye hifadhi ya Laikipia Nature Conservancy, ili kupigana na wimbi la uhalifu na mashambulizi ya wizi wa mifugo.
Kiunjuri ambaye ni mbunge wa zamani wa Laikipia Mashariki anasema kwamba kuwepo kwa maafisa wa usalama katika eneo hilo hakujatatua hali hiyo na kwa sasa polisi wa akiba ndiyo suluhu mwafaka la kukabiliana na majambazi hao.
Watu kumi na wawili wameuawa katika sehemu hiyo katika kipindi cha majuma matatu yaliyopita kufuatia mashambulizi ya majambazi.
Leave a Comment