Watu watatu wamepigwa risasi na kuuwawa na wezi wa mifugo katika kijiji cha Ndindika, wilaya ya Ngarua kaunti ya Laikipia.
Mtu mmoja alijeruhiwa pia katika jaribio la wizi wa mifugo kupitia hifadhi ya Laikipia Nature.
Kulingana na msemaji wa polisi Bruno Shiosi, Wavamizi hao walikuwa wametekeleza wizi wa mamia ya mifugo kutoka boma za wakaazi eneo hilo jana jioni mwendo wa saa kumi, lakini wakakabiliwa njiani na maafisa wa usalama.
Saa chache baadaye wavamizi hao waliweza kurejea kulipiza kisasi baada ya kugadhabishwa na kitendo cha maafisa hao kuwatwaa mifugo hao kutoka kwao.
Wavamizi hao kutoka Pokot waliingia kwenye boma la Michael Kananu na kutoweka na ng’ombe 32 na kondoo wawili, na njiani wakawapiga risasi watu wanne waliokuwa wakivua samaki kwenye bwawa la Mbogoini.
Kulingana na Shiosi, polisi hata hivyo walifanikiwa kuwakabili tena na wakapotea wakiacha nyuma mifugo hao waliorejeshewa mwenyewe.
Leave a Comment