Polisi katika kaunti ya Laikipia wanamzuilia jamaa mmoja anayetuhumiwa kuwashambulia mkewe, mama mkwe na jirani yao katika eneo la Marmanet kufuatia mzozo uliohusisha watoto.
Chistopher Mwaura ambaye alikuwa amesafiri kutoka jijini Nairobi hadi eneo la Maili Saba kaunti ya Laikipia anaripotiwa kushambulia watatu hao kwa kisu baada ya kukatazwa kuona watoto wake.
Inasemekana kwamba Mwaura alikusudia kuchukua watoto wake kutoka kwa mkewe Susan Wairimu ambaye amekuwa akiishi nao tangu watengane miezi miwili iliyopita.
Watatu hao wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Nyahururu huku mshukiwa akitiwa mbaroni na kusubiri kushtakiwa.
Leave a Comment