Baadhi ya shule zilizokuwa zimefungwa kwenye kaunti ya Laikipia kutokana na utovu wa usalama zilifunguliwa mapema leo.
Haya yalijiri baada ya maafisa zaidi wa usalama kutua kwenye kaunti hiyo kukabiliana na wahuni ambao wamekuwa wakiwahangaisha wakazi huku mashule yakipewa ulinzi wa kutosha.
Wikendi iliyopita inspekta generali wa polisi Hillary Mutyambai alitangaza kuwa hakuna mikutano ya kisiasa itakayo ruhusiwa kwenye kaunti hiyo kama njia moja ya kukabiliana na tatizo la utovu wa usalama.
Pia msemaji wa polisi Bruno Shioso alisema kuwa kwa sasa hali ya utulivu imeanza kurejea kwenye kaunti hiyo.
Leave a Comment