Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Thiru iliyoko Nyahururu kaunti ya Laikipia Shelmith Thimba na naibu wake David Maina wanazuiliwa na maafisa wa usalama mjini Nyahururu kwa tuhuma za kuwadhulumu wanafunzi watatu.
Inadaiwa kuwa naibu mwalimu mkuu David Maina ndiye aliyewafunga kwa kamba wanafunzi hao Kisha kuwapiga picha na kuzisambaza kwa walimu wenzake.
Akidhibitisha kukamatwa kwa wawili hao naibu Kamishna wa kaunti ndogo ya Nyahururu Moses Muroki ametupilia mbali madai kuwa walimu hao walikuwa wanawatumia wanafunzi hao Kama mfano wa kufunza katika mtaala mpya wa elimu CBC.
Leave a Comment