Watu wapatao 1,500 wanaoishi karibu na mji wa Nanyuki kaunti ya Laikipia, wameenda mahakamani kupambania kile wanachokiona kama jaribio la jeshi la Uingereza la kukwepa hatua za kisheria katika kesi ambayo walioshitaki ya kuuawa kwa wanyama na uharibifu wa mazingira wakati wanajeshi hao wanafanya mazoezi.
Makabiliano hayo ya mahakamani yalianza kutokana na shughuli za askari wa Uingereza waliokuwa wanafanya mazoezi katika hifadhi ya Lolldaiga miezi mitano iliyopita, huku ukiteketeza mimea kwenye ekari 12,000 na kukiwa na madai ya mtu mmoja kuuawa.
Kitengo cha mafunzo cha jeshi la Uingereza nchini Kenya kimewasilisha utetezi wao.
Waliopeleka mashtaka, wakiwemo wananchi na kituo cha ‘ African Centre for Corrective and Preventive Action’, wametaka watu walioathirika kulipwa fidia kutokana na uharibifu wa ardhi pamoja na hasara ya kifedha.
Mashtaka hayo yanadai wanyama pori walitoroka katika eneo lao la hifadhi na kuharibu nyumba zao, kuharibu mashamba yao na hata kuwasababishia athari ya kiakili.
Pia kulikuwa na madai ya mtu mmoja kufariki akijaribu kukabiliana na moto huo.
Mahakama ya mazingira mjini Nanyuki imetaja tarehe 26 mwezi ujao wa Oktoba, kama tarehe ya kusikiliza tetesi za pande zote mbili kabla ya kuendelea na kesi.
Leave a Comment