Wakulima kwenye eneo bunge la Bahati wameilaumu wizara ya mifugo kwenye kaunti ya Nakuru, kwa kukana madai kwamba hakuna mifugo ambao wamefariki kutokana na ugonjwa unaoadhiri kwato na midomo maarufu kama Foot And Mouth katika eneo hilo.
Wakiongea na Sauti ya Mwananchi katika eneo la Kamiruri wakulima hao wakiongozwa na John Kibe, wameeleza kupoteza mifugo wengi kutokana na ugonjwa huo, na hakuna usaidizi ambao wameweza kupokea kutoka kwa madaktari wa mifugo.
“Tegemeo letu ni mifugo hapa katika kaunti ya Nakuru,serikali ya Kaunnti na madaktari walikosa uadilifu ili kuzuia kupoteza mifugo wetu.” John Kibe akasema
Mkulima Paul Waweru ambaye pia aliadhirika na hali hiyo, amesema kuwa ni muhimu serikali ya kaunti iweze kuleta madaktari wa mifugo kutoka kaunti zingine iwapo hamna madktari wa kutosha kwenye kaunti.
“Tulipokua tukiuliza kwa nini Ngombe wamekufa Mbunge wa Bahati ambaye pia ngombe wake wamekufa amesema kuw serikali ya Kaunti ingefaa kutoa suluhu kabla ya maafa haya.”Paul Waweru Amesema
Leave a Comment