Walokuwa madiwani katika serikali za mbeleni wameitaka serikali kuhakikisha kutekelezwa kwa malipo yao ya kutuzwa kwa kazi yao ya shilingi milioni moja nukta tano kila mmoja ilivyokuwa makubaliano yao
Wakiongea mjini Nakuru kwenye kikao chao cha kila mwaka wakiongozwa na mwenyekiti na Meya wa zamani Samson Nkanata wanalalamikia kujikokota kwa shughuli nzima .
Wanasema kukawia kwa shughuli hiyo kumezidi kuwaathiri wengi wao ambao ni wakongwe kwa sasa na ambao idadi kubwa imeanza kupata changamoto za kiafya mbali na baadhi yao wameshaaga dunia.
Huku wakipongeza serikali ya kaunti ya Nakuru kwa juhudi zake kidogo za kuangalia maslahi ya viongozi hao katibu wao Geoffrey Mutai amesisitiza swala la wanakoegesha magari yao lafaa kuzidi kushughulikiwa wakiomba wabunge pia kuunga mkono shughuli hiyo na kuhakikisha wanasiasa hao wakongwe wanapokea haki zao.
Leave a Comment