Mahakama moja ya hapa Nakuru imesitisha ndoa ya mwanamme mmoja mkongwe ambaye alikuwa ameenda mahakamani akisema anafaa kufaidika na sehemu ya mahari iliyotolewa kwa bintiye, licha ya kutelekeza familia hiyo kwa miaka 27.
Joel Lagat Maina mwenye umri wa miaka 72, amepata pigo baada ya mahakama kumzuilia kugawa mahari ya bintiye.
Hakimu mkuu mkaazi Yvone Kathambi, amesema hakukuwa na mbinu hata moja ya kuokoa ndoa ya Langat kwa mkewe Joyce Chemutai mwenye umri wa miaka 65.
Hata hivyo hakimu Kathambi ametupilia ombi la Langat mahakamani kwa misingi halikuwasilishwa kwa njia inayofaa.
Wawili hao wamekuwa kwenye ndoa tangia mwaka wa 1992.
Leave a Comment