Mwalimu mmoja wa shule moja ya upili jijini Nairobi amefikishwa katika mahakama ya Kibera na kushtakiwa kwa kosa la kutumia wadhifa wake vibaya.
Dennis Otieno anatuhumiwa kujaribu kutongoza msichana wa miaka 15, kumguza vibaya na kumbusu kwa nguvu. Anadaiwa kutekeleza makosa hayo kati ya mwezi Julai mwaka jana na mwezi Septemba mwakani katika mtaa wa Dagoretti, Nairobi.
Kulingana na stakabadhi za mahakama, Otieno anadaiwa kutumia wadhifa wake kama mwalimu kutongoza mwanafunzi wake kwa kumguza kifua na kumbusu.
Otieno alisimamishwa kazi na kisha kukamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo alikanusha mashtaka dhidi yake na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi 100,000. Kesi hiyo itatajwa tena baadae mwezi huu.
Leave a Comment