Polisi katika kaunti ya Makueni wanamsaka jamaa mmoja anayedaiwa kumbaka mama yake mkongwe kisha kuenda mafichoni.
Patrick Mumo Ngenge (45) anaripotiwa kumbaka mama yake mwenye umri wa miaka (90) mida ya saa mbili usiku wa Jumatano nyumbani kwao katika eneo la Mbooni .
Maafisa wa DCI wameripoti kwamba ndugu mkubwa wa mshukiwa alipata mama yake akiwa anajikunja kutokana na maumivu huku akilalamika kuumwa na kiuno,.
Mhasiriwa alisimulia mwanawe mkubwa jinsi Mumo alivyoingia katika chumba chake cha malazi alipokuwa amelala na kujiburudisha na yeye kabla ya kutoweka.
Mkongwe huyo alikimbizwa katika hospitali ya Kisau akiwa hali mahututi ambako anaendelea kupokea matibabu. Ripoti za daktari zilithibitisha kwamba mhasiriwa alibakwa.
Polisi wametoa agizo kwa Mumo ajisalimishe katika kituo chochote kilicho karibu kabla ya wamkate wenyewe.
Leave a Comment