Waziri wa utalii Najib Balala ametetea kufanyika kwa mashindano ya magari ya dunia katika mbuga ya wanyama ya Hellsgate mjini Naivasha na kusema hayatakuwa na madhara yeyote kwa mazingira.
Akizungumza baada ya kuzuru mbuga hiyo, Balala amesema wataalamu wa maswala ya mazingira walikuwa wamefanya utafiti umedhihirisha kuwa wanyama walio mbugani hawataadhiriwa kwa vyovyote na mashindano hayo yatakayofanyika mwezi julai mwaka huu.
Vile vile waziri huyo amesema kuwa mashindano hayo yatakuwa ya kitaifa na yatawaleta takriban wageni laki moja mjini humo na kuongeza kuwa walikuwa wakishirikiana na muungano wa wasimamizi wa mashindano hayo ili kuhakikisha kuwa yatakuwa ya kufana.
Naye mwenyekiti wa muungano huo Phineas Kimathi amesema madereva kutoka kila kona ya ulimwengu watashindana katika mashindano hayo.
NA SILAS MWITI
Leave a Comment