Katibu kutoka wizara ya uchimbaji madini humu nchini John Omenge amesema serikali inapania kuweka mpango wa ramani katika maeneo kunakoshuhudia maporomoko ya ardhi msimu wa mvua. Hii ni baada ya mvua nyingi kuharibu madarasa kumi na moja na watu wanne kufariki katika eneo la Kapkonder.
“Tunatarajia kufananya maandalizi ili kuyalinda mazingira kutokana na maporomoko yanayotokea mara kwa mara ,tunajipanga kufanya uchunguzi wa kisayansi kubaini suluhisho la kudumu,tunawaomba wananchi kupanda miti katika mashamba yao.”John Omenge amesema.
Beatrice Koech
Leave a Comment