Kenya ilimaliza katika kilele cha jedwali la medali kwenye makala ya 18 ya Mashindano ya Dunia ya Vijana walio chini ya miaka 20 katika katika uwanja wa michezo wa kimataifa Moi Kasarani hapo jana
Kenya ilijizolea jumla ya medali saba jana -dhahabu tatu, fedha na shaba tatu.
Hiyo ilifikisha idadi ya medali za Kenya hadi 16; dhahabu nane, fedha moja na shaba saba, matokeo bora kabisa nchini kwa miaka 11 kwenye mashindano hayo ya vijana duniani.
Mafanikio ya wanamichezo wa Kenya kwenye mashindano hayo yalizidi matokeo waliosajili katika ubingwa wa mwaka wa 2,000 huko Santiago, 2006 mjini Beijing na 2010 huko Moncton.
Finland ilimaliza ya pili kwa medali tano -nne za dhahabu na moja ya fedha ilhali Nigeria ilimaliza ya tatu kwa medali saba -nne za dhahabu na tatu za shaba . Ethiopia ilifuata kwa dhahabu tatu, fedha saba na shaba mbili .
Leave a Comment