Mshindi wa medali ya shaba katika michezo ya Olimpiki mwaka wa 2020 kitengo cha riadha ya mita 1,500 Timothy Cheruiyot ameongezewa mamlaka na kuwa suparitenda mkuu wa kitengo cha magereza.
Awali alikuwa na cheo cha inspekta mkuu wa magereza, na kupandishwa kwake cheo kunafuatia amri ambayo ilitolewa na rais Uhuru Kenyatta hapo jana.
Zoezi hilo liliongozwa na kamishina mkuu wa kitengo cha magereza Wycliffe Ogallo katika makao makuu ya idara hiyo kwenye jumba la Magereza House.
Cheruiyot alijishindia fedha kwenye mashindano hayo baada ya kuibuka wa pili nyuma ya raia wa Norway Jakob Ingebrigtsen.
Leave a Comment