Mwanafunzi mmoja aliwasili bila chochote katika shule ya Upili ya Kanyawanga katika kaunti ya Migori kujiunga na kidato cha kwanza.
Kulingana na mwanafunzi huyo, juhudi za wazazi wake kumtafutia karo na bidhaa zingine za matumizi zilikua zimegonga mwamba.
John Otieno Odhiambo aliuza ndizi alizopanda akiwa mwanafunzi katika shule ya Msingi ya Ng’ong’a ili kupata Shilingi 100 alizotumia kama nauli kutoka Awendo kwenda shuleni.
Odhiambo alipata alama 337, akilenga kuwa daktari wa neva katika siku zijazo baada ya kumaliza chuo kikuu endapo atafaulu shule ya upili.
Leave a Comment