Familia ya mwanamke Phanice Awinja kutoka kaunti ya Bungoma inataka wizara inayoshulika na maswala ya nchi za kigeni almarauufu foreign affairs kuharakisha na kuwasaidia kumrejesha jamaa yao aliyeenda nchi ya saudia kufanya kazi ya uyaya na anapata mateso kutoka kwa waajiri wake.
Kulingana na Godfrey Wanga nduguye Phanice dadake sasa yuko katika afisi za mawakala ambao hushughulika na maswala ya kuwapeleka wafayakazi huko na hana nauli yoyote baada ya mwajiri wake kukataa kumlipa mshahara wa miezi mitatu aliyofanya kazi ya kumwosha mama mgonjwa wa waajiri wake.
Leave a Comment