Wanafunzi wa shule ya upili ya wasichana ya PCEA kambala katika kaunti ndogo ya Molo wamefanya mgomo usiku wa kuamkia leo.
Mamia ya wazazi alfajiri ya leo walifika shuleni humo wakitaka kujua hali ya watoto wao pamoja na chanzo cha mgomo huo.
Hata hivyo wazazi hao walizuiliwa nje ya lango kuu la shule hiyo huku maafisa wa usalama wakianzisha uchunguzi.
Maafisa wa usalama pamoja na wale wa elimu wakiongozwa na naibu kamishina Josphat Mutisya walifika kwenye mkutano shuleni humo huku wazazi wakielezea hisia zao kwa wanahabari nje ya lango la shule hiyo.
Habari zaidi itafuata…
Leave a Comment