Sajenti mmoja wa polisi alifikishwa mahakamani hii leo kule Mombasa kuhusiana na kifo cha mwanafunzi wa shule ya sekondari Tony Katana.
Katana alipigwa risasi na kuuawa na
sajenti John Otieno katika eneo la Uwanja wa Mbuzi Kongowea mjini Mombasa mwaka wa 2016.
Kufikia siku ya kifo chake, Katana alikuwa
na miaka 16 na alikuwa mwanafunzi wa
kidato cha pili katika shule ya upili ya Harvard mjini Mombasa.
Kati ya walioshuhudia ni akiwemo
wanafunzi pamoja na maafisa wa polisi waliokuwa kwenye doria usiku wakati
alipigwa risasi akielekea hafla moja ya sherehe.
Leave a Comment