Vilabu ambayo vitakiuka sheria msimu huu wa likizo na kuwauzia vileo watu chini ya umri vitafungwa na wahudumu wake kutiwa nguvuni na kuchukuliwa hatua za kisheria
Naibu kamishina kaunti ndogo ya Molo David Wanyonyi amesema hatua hiyo itatekelezwa bila huruma huku akiwataka wazazi kuwajibikia majukumu yao kwa watoto wao
Wanyonyi amesema watoto hupotoka kimaadili haswa wakati wa likizo jambo ambalo huwa changamoto kwa idara ya elimu shule zinapofunguliwa
“Itakua ni serikali dhidi yao kama watapatikana wakiwauzia watoto pombe ,tunawarai wauzaji wawe waangalifu zaidi msimu huu.”Alisema Wanyonyi
Leave a Comment